Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA

Côte d’Ivoire: Hatujaarifiwa tarehe ya kurudi kwa Gbagbo

Kulingana na msemaji wa serikali ya Côte d’Ivoire, Amadou Coulibaly, Juni 17, tarehe iliyotolewa na chama cha FPI-GOR kuhusu kurudi nchini kwa rais wa zamani Laurent Gbagbo haijafikiwa na pande husika. Tarehe hiyo haijafahamishwa mamlaka.

Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire Laurent Gbagbo..
Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire Laurent Gbagbo.. Jerry LAMPEN ANP/AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Je! Laurent Gbagbo atarudi nchini Cote d'Ivoire Juni 17? Ikiwa tarehe hiyo ilitangazwa kwa shangwe kubwa na katibu mkuu wa chama cha FPI-GOR, maafisa kadhaa wa serikali walishangaa kupata habari kupitia vyombo vya habari. Dakika chache baada ya tangazo hilo, Waziri wa Maridhiano ya Kitaifa, Kouadio Konan Bertin - mjumbe wa serikali katika mazunumzo na chama cha FPI juu ya utaratibu wa kurudi kwa Laurent Gbabo- ameihakikishia RFI kwamba hajafahamishwa kuhusu tarehe hiyo iliyotangazwa.

Msemaji wa serikali Amadou Coulibaly, ambaye pia alimehojiwa na RFI, aanasema amesikitishwa kuona uamuzi huu unachukuliwa na upande mmoja. "Tulichokubaliana ni kwamba tarehe inapaswa kuwekwa wazibaada ya pande mbili kuafikiana, kwa hivyo kwetu tarehe hiyo aina nafasi yoyote," ameonya. Waziri wa Mawasiliano ametilia shaka uwezekano wa kurudi kwa Laurent Gbabo nchini Côte d’Ivoire : "Sijui angefikaje kwa tarehe hii ya Juni 17 ikiwa hakuna mipango yoyote inayofanywa kwa mapokezi yake".

Tangu Aprili, mazungumzpo kati ya kamati ya mapokezi ya Laurent Gbagbo na serikali yamejikita katika kupata makazi ya rais wa zamani au hata utaratibu wa mapokezi kwa raia kwa kiongozi huyo wa zamani, ambaye bado ana wafuasi wengi nchini.

Mwanzoni mwa mwezi Aprili, Rais wa Côte d’Ivoire Alassane Ouattara alisema kwamba Laurent Gbagbo anaweza kurudi "wakati wowote anapotaka", na kwamba atalipiwa gharama zake za usafiri. Lakini kulingana na msemaji wa serikali, tarehe ya kurudi kwa kwake nchini ilipaswa kuafikiwa kati ya pande zote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.