Pata taarifa kuu
CHAD-UHUSIANO

Kiongozi wa Chad Mahamat Idriss Deby ziarani Niger

Hii ni ziara yake ya kwanza nje ya Chad tangu alipochukua nafasi ya mkuu wa Baraza la Kijeshi. Mahamat Idriss Déby Itno yuko Niger Jumatatu hii, Mei 10.

Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno kwenye mazishi ya baba yake, Idris Déby Itno, Aprili 23, 2021.
Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno kwenye mazishi ya baba yake, Idris Déby Itno, Aprili 23, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Amekwenda kukutana na wanajeshi wake katika kanuti ya Tera, lakini pia alipowasii amezungumza na viongozi wa ngazi ya juu wa Niger.

Wakati huo huo, jeshi la Chad lmeatangaza kumalizika kwa operesheni za kijeshi dhidi ya waasi wa Front for Alternation and Concord in Chad (FACT)

Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno aliwasili mapema asubuhi huko Niamey, ameripoti mwandishi wetu huko Niamey, Moussa Kaka. Amepokelewa na Waziri Mkuu wa Niger, Ouhoumoudou Mahamadou. Baada ya hapo amekutana kwa mazungumzo na Rais Bazoum Mohamed katika ukulu ya rais ya mjini Niamey.

Akifuatana na wanachama wengine wa Baraza la Kijeshi la Mpito, wote wakiwa wamechoka, Jenerali Mahamat Idriss Déby alifanya mahojiano marefu na Rais Mohamed Bazoum. Alitangaza kwenye redio ya serikali kwamba amekuja kuimarisha uhusiano wa urafiki kati ya nchi yake na Niger, kufanya mazungumzo na Rais Bazoum Mohamed, mpatanishi kwa niaba ya G5 Sahel katika mgogoro huo wa Cad, na kutoa rambirambi kwa wanajeshi 1,200 wa Chad, kufuatia kifo cha Marshal wa Chad, aliyeuawa akiongoza mapigano dhidi ya waasi magharibi mwa Niger kwenye mipaka hiyo mitatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.