Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA

Chad: Hali yazidi kuzorota kando na maandamano dhidi ya mamlaka

Kumetokea machafuko Jumamosi hii asubuhi katika maeneo kadhaa ya Ndjamena, mji mkuu wa Chad. Vyanzo kadhaa vinabaini kwamba watu kadhaa wamejeruhiwa, na wengine wengi kukamatwa.

Makabiliano huko Ndjamena, Aprili 27, 2021 (picha ya zamani).
Makabiliano huko Ndjamena, Aprili 27, 2021 (picha ya zamani). AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati muungano wa kiraia wa Wakit Tama ulikuwa umeitisha maandamano dhidi ya mamlaka Jumamosi hii, mamlaka ambayo wanasema iko kinyme cha sheria.

Mapema asubuhi hali ilikuwa shwari na ghafla hali ilibadilika na kushuhudiwa kwa machafuko karibu saa 12:45 asubuhi (saa za Chad).

Maafisa wa polisi waliwafyatulia risasi za moto waandamanaji waliokuwepo kwenye eneo lililotengwa na waandaaji wa maandamano katika eneo la Fest Africa katika Kaunti ya 6. Mashahidi wanasema maafisa wa polisi walifyatua hovyo risasi za moto. Majeruhi wawili walisafirishwa  hospitalini na watu tisa wamekamatwa, kulingana na viongozi wa muungano wa kiraia wa Wakit Tama.

Mandamano kama hayopia yamefanyika katika maeneombalimbali ya mji wa Ndjamena, ikiwa ni pamoja na Walia na Atrone.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.