Pata taarifa kuu
CHAD-SIASA

Chad: Muungano wa kiraia wa Wakit Tama waitisha maandamano mapya Jumamosi

Siku mbili baada ya kutangazwa kwa serikali ya mpito, iliyotangazwa na viongozi wapya kama serikali ya umoja, muungano wa mashirika ya kiraia umekutana Jumanne hii.

Ikulu ya rais Chad, katika eneo la Djambel Bahr, Ndjamena, mai 2021.
Ikulu ya rais Chad, katika eneo la Djambel Bahr, Ndjamena, mai 2021. © David Baché
Matangazo ya kibiashara

Muungano huu, Wakit Tama, unaoundwa na mashirika ya kiraia na vyama vya siasa vya upinzani, ambao unaongoza maandamano ya kiraia dhidi ya mamlaka mpya za mpito.

Muungano wa Wakit Tama umekutana Jumanne hii asubuhi kutoa wito wa kufanyika kwa maandamano mapya Jumamosi hii, kwa siku nne. Viongozi wa muungano huo wa kiraia wanatazamia kuendelea na hata kuongeza nguvu katika mapambano yao.

Kwa pande wao, serikali ya mpito ambayo ilitangazwa Jumapili jioni sio serikali ya umoja. Wanaeleza kuwa kwa vile wanakapina Baraza la Kijeshi la Mpito - wanajeshi hawa kumi na tano wanaongozwa na Mahamat Idriss Déby, mtoto wa hayati rais Idriss Déby, ambaye anaongoza nchi - kila kitu ambacho Baraza hili la Jeshi linafanya, kwa mujibu wao, ni haramu. Kwa hivyo hakuna swali la kuitambua serikali mpya.

Sehemu ya upinzani yashiriki katika serikali ya mpito

Hata hivyo vyama vingine vya upinzani vimeamua kujiunga na serikali hii ya mpito, vyama ambavyo kwa kwa wakati fulani vilishiriki maandamano dhidi ya Baraza la Kijeshi la Mpito. "Wamefukuzwa katika muungano wetu," viongozi wa Wakit Tama wamesema kwa kauli moja, huku wakidhiirisha hasira zao.

Wanachama wa Wakit Tama wanataka kuendelea kulaani, mitaani, kile wanachotaja kama "mapinduzi ya taasisi". Wanadai kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba na kufunguliwa kwa mazungumzo ya kweli ya kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.