Pata taarifa kuu
AFRIKA-AFYA

Afrika yafanya majaribio mapya ya kliniki katika vita dhidi ya Malaria

Malaria iliua karibu watu 400,000 duniani mwaka wa 2019, wengi akiwa ni watoto walio na umri wa chini ya miaka 5. Ingawa Malaria ni ugonjwa unaoua , inaweza kutibiwa kwa dawa ya artemisinin-iliyochanganywa na dawa nyingine.

Malaria ni ugonjwa unaoweza kusababisha kifo, ambao uliua watu 400,000 duniani mwaka wa 2019.
Malaria ni ugonjwa unaoweza kusababisha kifo, ambao uliua watu 400,000 duniani mwaka wa 2019. iStock / RolfAasa
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo tatizo la matibabu haya ni kwamba vimelea huwa vinajidhatiti mara kwa mara. Kwa hivyo baadhi ya watafiti wanafanya kazi juu ya utengenezaji wa dawa mpya na majaribio kwa sasa yanafanywa kwa watoto 1,600 walio na umri wa chini ya miaka 5 nchini Mali, Ghana, Gabon na Benin ...

Majaribio ya kitabibu yaliyofanywa katika nchi hizi nne za Kiafrika yanajaribu kuonyesha ufanisi wa dawa ya mseto ya artemisinin iliyochanganywa kwa dawa tatu badala ya mbili kama ilvyokuwa hapo awali.

"Lengo la mradi huo ni kutoa uthibitisho kwamba matumizi ya dawa hizi tatu ni mazuri na yenye ufanisi na inastahimiliwa vizuri na wagonjwa, inamaanisha ina athari chache za ziada ikilinganishwa na mchanganyiko wa dawa mbili, na kutokuwepo kwa hali mbaya katika viwango vya dawa za plasma," anaeleza mtafiti Jérôme Clain, ambaye alianzisha majaribio haya.

Mchanganyiko wa dawa tatu watokomeza vimelea sugu

Matumizi ya dawa tatu ni matibabu, kama jina lake linavyopendekeza, kulingana na molekuli tatu. Ya kwanza, artemisinin huondoa vimelea vingi katika muda wa saa chache, ya pili inaendelea kutokomeza na ya tatu inaimarisha ya pili kwa kuua vimelea sugu.

Malaria inabakia kuwa tishio kubwa kwa afya ya umma. Vifo tisa kati ya kumi vinatokea barani Afrika na wengi kati hao ni watoto chini ya miaka mitano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.