Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu visa vya ubakaji katika jimbo la Tigray

Umoja wa mataifa pamoja na mashirika ya kutoa misaada , yameonya hali ya kibinadamu katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia ,inazidi kuwa mbaya na  hakuna ushahidi kuwa wanajeshi wa  Eritrea kuondoka eneo hilo.

Lowcock ameliambia Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa  kuwa mapigano bado yanaendelea katika jimbo la Tigray lakini pia wanawake na wasichana wanabakwa pamoja na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu..
Lowcock ameliambia Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa mapigano bado yanaendelea katika jimbo la Tigray lakini pia wanawake na wasichana wanabakwa pamoja na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu.. EDUARDO SOTERAS AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mkuu wa mashirika ya kutoa msaada, Mark Lowcock, amesema licha ya waziri mkuu Abbiy Ahmed kutangaza kuwa wanajeshi wa Eritrea wanaondoka katika jimbo hilo, mpaka sasa hakuna ushahidi kuwa hilo linafanyika.

Aidha, Lowcock ameliambia Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa  kuwa mapigano bado yanaendelea katika jimbo la Tigray lakini pia wanawake na wasichana wanabakwa pamoja na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wiki hii, shirika la kimataifa la kutetea haki za binadaam ,la Amnesty International ,liliripoti kuwawuwa kwa watu watatu waliowauwa na wanajeshi wa Eritrea  huku wengine 19 wakijeruhiwa kwenye jimbo la Tigray.

Hii sio mara ya kwanza kwa wajumbe wa Baraza la Usalama kuelezwa kinachotokea katika jimbo la Tigray lakini haijatoa msimamo wa pamoja kuhusu mzozo huo ulioanza mwezi Novemba mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.