Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lagawanyika kuhusu Tigray

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana alhamisi wiki hii jijini New York kujadili hali inayojiri katika jimbo la Tigray, nchini Ethiopia, ambapo kulingana na Umoja wa Mataifa hali inazidi kuwa mbaya.

Mooja wa wakaazi huko Wukro, kaskazini mwa mji wa Mekele katika jimbo la Tigray? Machi 1, 2021.
Mooja wa wakaazi huko Wukro, kaskazini mwa mji wa Mekele katika jimbo la Tigray? Machi 1, 2021. AFP - EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya tano Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoelewana kuhusu hali huko Tigray tangu kuzuka kwa mgogoro mwezi Novemba mwaka jana.

Hali ya kibinadamu ilitawala sehemu kubwa ya kikao hicho- na wanadiplomasia walishtushwa na ripoti za visa vya ubakaji vinavyotekelezwa na watu wanoshukiwa kuwa vikosi vya ulinzi na usalama vya serikali, huku raia wakikabiliwa na njaa.

Baraza hilo limegawanyika, kwa upande mmoja Urusi, China, Kenya, ikiungwa mkono na nchi za Kiafrika wanachama wa Baraza hilo, ambao wanabaini kuwa Addis Ababa tayari imefanya juhudi kwa kuruhusu mashirika ya kutoa misaad akuingia katika jimbo la TIgray na wito wake wa kuondoka kwa Eritrea katika jimbo hilo.

Kwa upande mwingine, nchi za Magharibi ambazo zinadai kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa maazimio ya Ethiopia, na kuanza - kwa baadhi- kukosa subira. Marekani, ikishtushwa na ukosefu wa umoja kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, imetaka kutumia njia nyingine ya kuishawishi erikali ya Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.