Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-UNHCR

Ethiopia: UNHCR yatiwa wasiwasi juu ya hatima ya wakimbizi

Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu hatimaye limeweza kuingia katika jimbo la Tigray, Kaskazini mwa Ethiopia, ambalo linakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kibinadamu uliosababishwa na vita kati ya jeshi la shirikisho na vikosi vya TPLF.

Vikosi vya Jeshi nchini Ethiopia
Vikosi vya Jeshi nchini Ethiopia Tiksa Negeri/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, malori saba yaliyobeba vifaa vya matibabu yaliwasili Jumamosi hii, Desemba 12 huko Mekele, mji mkuu wa jimbo la Tigray, zaidi ya mwezi mmoja baada ya kuzuka kwa uhasama huo.

Msafara huo ulikuwa umebeba dawa na vifaa vya matibabu kutibu zaidi ya watu 400 waliojeruhiwa pamoja na vifaa vya matibabu ya magonjwa ya kawaida na sugu.

Msaada huo umepewa Hospitali ya Ayder, hospitali kuu ya Mekele, Ofisi ya Afya ya kikanda na duka la dawa linalomilikiwa na shirika la Msalaba Mwekundu katika mji huo .

Zaidi ya yote, malori haya yatasaidia kufungua hospitali kuu ya Mekele, ambayo imejaa watu waliojeruhiwa, kama Jeremy England, mkuu wa shughuli wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu anasema.

"Madaktari wanakabiliwa na uchaguzi mbaya," anaelezea. Wanapaswa kupanga wagonjwa, kati ya wale wanaoweza na hawawezi kutibu. Wanachagua kulingana na nyenzo wanazopata, kulingana na kupunguzwa kwa umeme na uwezo wao wa kuzuia vifaa kati ya shughuli. "

80% ya wagonjwa wanaaminika kujeruhiwa vitani. Shughuli za matibabu zimekuwa ngumu katika mji ambao unakabiliwa na uhaba wa dawa chakula, umeme  na maji safi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.