Pata taarifa kuu
MOROCCO-SAHRAWI-USALAMA

Sahara Magharibi: Morocco yazindua operesheni ya kijeshi katika eneo la Guerguerat

Vikosi vya jeshi la Morocco vimeanzisha operesheni ya kijeshi leo Ijumaa katika eneo la mpakani huko Guerguerat dhidi ya vikosi vya Polisario Front, vikishtumu kundi hilo kuanza chokochoko. Eneo la mpakani huko Guerguerat limefungwa kwa wiki kadhaa sasa.

Askari wa jeshi la Morocco, akiwa katika mafunzo (picha ya kumbukumbu).
Askari wa jeshi la Morocco, akiwa katika mafunzo (picha ya kumbukumbu). Source Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati waliojitenga wa Polisario Front walikuwa wameonya kwa siku kadhaa. Walitishia kujibu kwa kuingiza vikosi vyake katika eneo la Guerguerat.

Leo Ijumaa asubuhi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sahrawi, Mohamed Salem Ould Salek, amebaini kwamba hatua za Morocco ni za uchokozi na kutangaza kuwa wako katika hali ya kujihami. Ameongeza kuwa "vita vimeanza". Ameishutumu Morocco kwa "kukiuka makataba wa kusitisha mapigano" uliyosainiwa karibu miongo mitatu iliyopita, mnamo mwaka 1991, baada ya vita vya miaka 16.

Kwa upande wake, Morocco imedai kujibu hali hiyo huko Guerguerat. Lengo lake ni kufungua barabara katika eneo hilo inayoelekea Mauritania na ambayo pia ni barabara inayoelekea katikakanda ya Afrika Magharibi.

Wizara ya Mambo ya nje ya Morocco inashtumu Polisario Front na vikosi vyake kwa kufanya vitendo vya ujambazi na inafikiria kuanzisha mùashambulizi kujibu dhidi ya uchokozi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.