Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: Karibu wanajihadi hamsini wauawa katika operesheni ya kikosi cha Barkhane

Waziri wa Jeshi wa Ufaransa, Florence Parly amefanya ziara ya saa chache huko Bamako, nchini Mali, Jumatatu Novemba 2. Alikutana na mamlaka mpya za Mali.

Vikisaidiwa na ndege za kivita aina ya Mirage 2000s kutoka Niamey na angalau ndege moja isiyokuwa na rubani aina ya Reaper, vikosi maalum vya Barkhane, vikishirikisha na makomandoo kadhaa walizindua operesheni kabambe dhidi ya wanajihadi.
Vikisaidiwa na ndege za kivita aina ya Mirage 2000s kutoka Niamey na angalau ndege moja isiyokuwa na rubani aina ya Reaper, vikosi maalum vya Barkhane, vikishirikisha na makomandoo kadhaa walizindua operesheni kabambe dhidi ya wanajihadi. Reuters/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ufaransa ametangaza kuwa Paris kwa ushirikiano na Bamako itaendelea na mapambano dhidi ya ugaidi, vita dhidi ya ugaidi ambayo imeanza kuzaa matunda. Mwishoni mwa mwezi Oktoba, karibu wanamgambo hamsini wa Kiislamu waliuawa kaskazini mwa Mali, alisema waziri huyo wa Ufaransa.

Baada ya kukutana kwa mazungumzo na rais wa mpito wa Mali Bah N'Daw, Waziri wa Jeshi wa Ufaransa alitoa maelezo juu ya utendaji wa kikosi cha Barkhane ambacho hivi karibuni kiliwauwa karibu wanamgambo hamsini wa Kiislamu kaskazini mwa Mali. eneo linalojulikana kama "mipaka mitatu".

"Ningependa kupongeza operesheni yenye umuhimu mkubwa ambayo ilifanywa mnamo Oktoba 30 nchini Mali na kikosi cha Barkhane na katika operesheni hiyo zaidi ya wanajihadi 50 waliangamizwa na pia kukamata vifaa vya kundi hilo lenye mafungamano na Al-Qaeda, ambalo lilipata pigo kubwa. "

Makao makuu ya jeshi la Ufaransa yamesema kuwa operesheni hiyo ilifanyika karibu na mkoa wa Mali wa Boulikessi usiku wa Oktoba 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.