Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAANDAMANO-USALAMA

Mgogoro wa Nigeria: Rais Buhari akutana kwa mazungumzo na watangulizi wake

Wakati mgogoro unaendelea nchini Nigeria, rais waNigeria Muhammadu Buhari amekutana kwa mazungumzo na watangulizi wake, ikiwa ni pamoja na Goodluck Jonathan na Olusegun Obasanjo, kuhusu hali ya usalama inayoendelea nchini humo.

Baada ya machafuko nchini Nigeria, rais Muhammadu Buhari amekutana kwa mazungumzo na wakuu wote wa zamani wa nchi hiyo ambao bado wako hai, kuhusu usalama.
Baada ya machafuko nchini Nigeria, rais Muhammadu Buhari amekutana kwa mazungumzo na wakuu wote wa zamani wa nchi hiyo ambao bado wako hai, kuhusu usalama. © Nigeria Presidency
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais, rais Buhari kwa mara nyingine amesikitishwa kuona maandamano ya amani ya vijana "yalivamiwa" na "majambazi" na " kugeuka kuwa ya vurugu".

Hapa waangalizi na waandamanaji wanaamini zaidi kuwa mamlaka ndio waliotumia na kuyapa silaha makundi ya majambazi ili kusambaratisha maandamano yao na kuishtumu serikali kuwa imehusika katika ukandamizaji huo uliosababisha maafa makubwa, amebaini rais Buhari.

Katika mkutano huo, ambao pia ulihudhuriwa na wakuu wa vyombo vya usalama vya Nigeria, Muhammadu Buhari alisisitiza kwamba alijibu madai ya waandamanaji, akiahidi, pamoja na mambo mengine, mageuzi ya polisi.

"Kwa bahati mbaya, (waandamanaji) wamekataa kusitisha maandamano yao na kufanya mazungumzo na serikali," alisikitika rais wa Nigeria, ambaye bado hajasema neno hata moja kuhusu ukatili wa jeshi siku ya Jumanne usiku huko Lagos.

Mkutano huu ni dhahiri ulikusudiwa kuonyesha uungwaji mkono wa wakuu wa zamani wa nchi. Rais wa zamani Olusegun Obasanjo, ambaye alimsihi rais azungumze mapema Jumatano, alimsifu Muhammadu Buhari kwa "hotuba yake jana usiku." "Hoja zako zilikuwa sahihi na zilistahili kukaribishwa," alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.