Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAANDAMANO-USALAMA

Nyota wa Nigeria wapinga vurugu za polisi

Nigeria inaendelea kukumbwa na hali ya wasiwasi tangu vikosi vya ulinzi kusambaratisha maandamano ya amani kwa nguvu za kupita kiasa na kusababisha vifo vya watu wengi Jumanne wiki hii.

Nigeria, Lagos Oktoba 21, 2020: waandamanaji bado wanaendelea na maamndamano.
Nigeria, Lagos Oktoba 21, 2020: waandamanaji bado wanaendelea na maamndamano. UnEarthical/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya kimataifa imelaani vurugu hizo na kwenye mitandao ya kijamii wito wa kumtaka rais Buhari kujiuzulu umeendelea kutolewa, hasa na nyota wa muziki nchini Nigeria kama vile Wizkid, Davido na Tiwa Savage.

Nyota wa Nigeria wanachukua nafasi muhimu katika maandamano haya. Wizkid amehutubia umati wa watu katika maandamano huko London, huku Davido akionekana kushirikiana na waandamanaji huko Abuja.

Wakati huo huo jeshi nchini Nigeria limekanusha ripoti kuwa iliwapiga risasi waandamanaji siku ya Jumanne katika mji wa kibiashara wa Lagos wakati wakiendeleza maandamano ya amani ya kutaka mabadiliko katika jeshi la Polisi, huku serikali nchini humo ikisema zaidi ya watu 20 walijeruhiwa. 

Walioshuhudia tukio hilo la waandamanaji kushambuliwa wanasema, maafisa hao wa usalama waliwalenga zaidi ya watu Elfu Moja, huku Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International likisema kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha na inatafuta idadi kamili lakini gavana Babajide Sanwo-Olu anasema hakuna mwandamanaji yeyote aliyeuawa.

Maandamano hayo yamekuwa yakiendendelea kwa wiki mbii sasa, huku waandamanaji wakitaka mageuzi katika jeshi la pôlisi na wameapa kutoacha harakati hizo.

Hii ni mara ya kwanza kwa waandamanaji nchini Nigeria hasa vijana kwa zaidi ya wiki mbili sasa kushinikiza mabadiliko katika jeshi la polisi na kupinga kikosi maalum kinachofahamika kama SARS kukabili uhalifu kwa kile wanachodai polisi wameendeleza unyanayasaji.

Serikali jijini Abuja, imekuwa ikiahidi mageuzi hayo, lakini waandamanaji wanaonekana kutoamini ahadi hiyo na wanamtaka rais Muhammadu Buhari kulizungumzia suala hili, wakati huu bunge likisema halitapitisha bajeti ya fedha hadi pale matakwa ya waandamanaji yatakapotatuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.