Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAANDAMANO-USALAMA

Jeshi la Nigeria latahadharisha waandamanaji

Jeshi la Nigeria limewaonya waandamanaji kuacha vitendo vinavyotishia amani na usalama wa nchi hiyo, wakati maandamano yakiendelea kushinikiza mageuzi katika jeshi la polisi na kufutwa kabisa kwa kikosi maalum cha kupambana na wahalifu SARS.

Maandamano yaendelea Nigeria, kulaani dhuhuma zinazodaiwa kufanywa na jeshi la Polisi nchini humo.
Maandamano yaendelea Nigeria, kulaani dhuhuma zinazodaiwa kufanywa na jeshi la Polisi nchini humo. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Maandamano yameendelea katika miji mikuu ya nchi hiyo Abuja na Lagos, huku waandamanaji wakidai kushambuliwa na watu wasiojulikana.

Uongozi wa jiji kuu Abuja, sasa umepiga marufuku maandamano hayo.

Maandamano yameendelea kushuhudiwa nchini Nigeria, kulaani dhuhuma zinazodaiwa kufanywa na jeshi la Polisi nchini humo, licha ya serikali kuahidi, kulifanyia mageuzi na kuvunjwa kwa kikosi maalum cha SARS kilichokuwa kimepewa kazi ya kupambana na wahalifu.

Mapema wiki hii serikali ilisema ina nia ya dhati ya kulifanyia mageuzi jeshi hilo, kauli ambayo imeungwa mkono na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Edward Kallon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.