Pata taarifa kuu
GUINEA-UCHAGUZI

UCHAGUZI GUINEA: Je ni rais Alpha Conde au kinara wa upinzani, Cellou Dalein Diallo

Raia nchini Guinea, wanapiga kura katika uchaguzi wenye utata, ambapo rais Alpha Conde, mwenye umri wa miaka 82, anawania kwa muhula watatu. 

Rais wa Guinea, Alpha Conde, akiwa katika moja ya mikutano yake mjini Conakry
Rais wa Guinea, Alpha Conde, akiwa katika moja ya mikutano yake mjini Conakry AFP
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la upigaji kura lilianza huku mvua kubwa ikinyesha kwenye maeneo mengi ya nchi, lakini misururu ya watu bado ilionekana katika vituo vya kupigia kura. 

Rais Conde, alikaidi ukosolewaji wa kutoifanyia marekebisho katiba, ambapo iliruhusu awanie kwa muhula watatu. 

Mpinzani mkuu wa rais Conde ni Cellou Dalen Diallo, ambaye alishindwa mara mbili katika chaguzi zilizopita. 

Vurugu za kikabila zilizoshuhudiwa wakati wa kipindi cha kampeni, zimezusha hofu ya kutokea machafuko nchini humo, ikiwa matokeo ya uchaguzi huu yatavurugwa. 

Serikali imetangaza kufungw     a kwa mipaka yake na baadhi ya nchi jirani, ikisema hatua hiyo ni kwa sababu za kiusalama. 

Zaidi ya wapiga kura milioni 5 wanashiriki uchaguzi huu, ambao matokeo yake yanatarajiwa kutolewa ndani ya siku chache zijazo baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika. 

Wagombea wanahitajika kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote ili kutangazwa mshindi, au vinginevyo kutalazimika kuwa na duru ya pili ambayo itafanyika November 24. 

Wagombea wengine 10 pia wanawania kiti hicho, huku baadhi ya wapinzani wengine walikuwa wametoa wito wa uchaguzi huu kususiwa. 

Hofu ya mgawanyiko ndani ya jeshi. 

Nchi ya Guinea kwa miaka kadhaa imeshuhudia ikitawaliwa kwa mkono wa chuma au na wanajeshi tangu ipate uhuru wake.  

Kumekuwa na wasiwasi kuwa huenda jeshi likaingilia tena siasa za nchi hiyo. 

Siku ya Ijumaa, waziri wa ulinzi alitoa taarifa kuthibitisha kuwa kikundi cha wanajeshi kilivamia kambi ya kijeshi ya Kindia, iliyoko umbali wa kilometa 130 mashariki mwa mji mkuu Conakry, na kumuua kiongozi wa kambi hiyo, Kanali Mamady Conde. 

Taarifa nchini humo zinadai kuwa huenda baadhi ya wanajeshi wanapanga kuasi na kuchukua nchi, licha ya kuwa mamlaka baadae zilidai kuwa wanajeshi waliovamia kambi hiyo ya kijeshi walidhibitiwa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.