Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: Mateka wa Ufaransa, Italia na Mali waachiliwa kutoka mikononi mwa wanajihadi

Sophie Petronin, mfanyakazi wa mashirika ya misaada, raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 75, aliyetekwa mwaka 2016 amewasili jiini Bamako pamoja na mwanasiasa wa nchini Mali, Soumaila Cisse.

Mateka wa zamani wa Ufaransa Sophie Pétronin pamoja na rais wa mpito wa Mali Bah N'Daw, katika ikulu ya rais huko Bamako, Oktoba 8, 2020, baada ya kuachiliwa.
Mateka wa zamani wa Ufaransa Sophie Pétronin pamoja na rais wa mpito wa Mali Bah N'Daw, katika ikulu ya rais huko Bamako, Oktoba 8, 2020, baada ya kuachiliwa. Présidence malienne / AP
Matangazo ya kibiashara

Pétronin amekuwa akielezwa kuwa mateka wa mwisho wa Ufaransa kushikiliwa popote duniani.

Furaha na nderemo ilijawa nyuso za ndugu jamaa na marafiki wa mateka hao wa zamani walipowasili jijini Bamako kwa ndege ya jeshi la Mali wakitokea katika mji wa Tessalit. Sophie Pétronin mfanyakazi wa mashirika ya misaada, alitekwa miaka minne iliopita, wakati mwanasiasa Soumaila Cisse akiwa mikononi mwa watekaji kwa kipindi cha miezi Sita.

Kwa mujibu wa ripota wa RFI jijini Bamako Serge Daniel, Sophie Petrona alionekana akishuka mwenyewe kwenye ndege na kukutana na mwanae Sebastien Chadaud Pétronin ambapo alisikika akilalamika “Mama, Mama”, huku akimfuata.

Wakati huo huo Soumaila Cisse alionekana akishuka kwenye ndege akivalia Barakoa na kukumbatiana na ndugu jamaa na marafiki.

Mateka hao wa zamani baadae walielekea katika Ikulu ya rais ilipo Kuoulouba ambako wamekutana na rais wa kipindi cha mpito Bah N'Daw, na baadae Sophie Petrona aliekea ubalozi wa Ufaransa, wakati ndege maalum ikiagizwa kumsafirisha mpaka Ufaransa ambako rais Emmanuel Macron atakutana na mwanamama huyo mfanyakazi wa mashirika ya misaada.

wakati huo huo, Serikali ya Mali imetangaza kuachiliwa huru kwa Waitaliano Nicola Chiacchio na Pier Luigi Maccalli. Majina yao yalikuwa hayajawahi kuonekana hadi wakati wanapoachiwa huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.