Pata taarifa kuu
MALI-SIASA-USALAMA

Mali: Jeshi lamuachilia huru Waziri Mkuu wa zamani Cissé na maafisa wengine

Waziri Mkuu wa zamani wa Mali Boubou Cissé na maafisa wengine wa kisiasa na kijeshi waliokamatwa katika mapinduzi ya Agosti 18 wameachiliwa huru, Makamu wa rais wa Mali Kanali Assimi Goïta amesema.

Waziri Mkuu wa zamani wa Mali Boubou Cissé
Waziri Mkuu wa zamani wa Mali Boubou Cissé REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kuachiliwa kwa viongozi hao wa zamani ilikuwa moja ya madai ya jamii ya kimataifa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), ambayo siku ya Jumanne iliondoa vikwazo vilivyowekewa nchi ya Mali baada ya mapinduzi ya Agosti 18.

Jamii ya kimataifa ilihofia kwamba mapinduzi hayo yangelisababisha kuzorota kwa hali ya usalama katika nchi zingine za ukanda huo , hali ambayo ingelisababisha athari kwa juhudi za mapambano dhidi ya wanajihadi katika eneo la Sahel.

Kanali Assimi Goïta, ambaye aliongoza mapinduzi, ameendelea kusalia katika uongozi wa nchi kama makamu wa rais anayesimamia maswala ya usalama na ulinzi, licha ya kuundwa kwa timu ya mpito inayohusika na kuongoza nchi kuelekea uchaguzi huru baada ya Rais Ibrahim Boubacar Keïta kutimiliwa mamlakani.

Moussa Timbiné, aliyekuwa spika Bunge la kitaifa lililovunjwa, na pia majenerali wanane ni miongoni mwa walioachiliwa huru, kulingana na taarifa iliyotolewa Jumatano na makamu wa rais wa Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.