Pata taarifa kuu
DRC-IMF-UCHUMI

DRC: Mazungumzo na IMF kwa mpango rasmi

Shirika la Fedha la Kimataifa limekamilisha ukaguzi wake wa utendaji kaezi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Kati ya mwezi Novemba na Mei, nchi ilikuwa chini ya uangalizi wa taasisi ya Bretton Woods kama sehemu ya mpango wa ufuatiliaji.

Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nje ya jengo la makao makuu huko Washington, Marekani.
Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nje ya jengo la makao makuu huko Washington, Marekani. REUTERS/Yuri Gripas/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Lengo lilikuwa kuboresha utawala na kuandaa Kinshasa kwa mazungumzo ya mpango wa miaka mitatu na kupewa msaada mkubwa.

DRC ililazimika kuanzisha mageuzi na kuboresha viashiria ili kutumaini kupata msaada wa IMF. Walakini, matokeo bado yako mbali na alama inayotarajiwa "ya kuridhisha kwa jumla", ambayo inaweza kuchelewesha au kuzuia kutia saini kwa mpango wa miaka mitatu.

Kwanza, ilichukua muda kwa Kinshasa kuacha kufanya shughuli yoyote inayohusiana na masuala ya kibenki. Hadi mwezi Aprili mwaka huu, benki kuu ilikuwa ikiikopa serikali pesa ili kuzuia upungufu wake na hii ilikuwa na athari mbaya kwa kiwango cha ubadilishaji na mfumko wa bei.

Tangu wakati huo, na hii ni hatua nzuri ambayo IMF inapaswa kutambua, Benki kuu ya DRC (BCC) na serikali walisaini makubaliano ya kusitisha shughuli hiyo na wanashikamana nayo hadi leo. Lakini pia ni kutokana na msaada wa bajeti wa zaidi ya dola Milioni 360 uliyotolewa na IMF mwishoni mwa mwezi Aprili ambao ulizuia pengo katika matumizi ya umma.

Kutokana na ongezeko la muswada wa mshahara unaohusiana na hatua ya elimu ya bure katika shule za msingi za umma, DRC pia ilijikubalisha kuboresha mapato yake. Kama inavyotarajiwa, serikali ilipanua wigo wa ushuru wa mapato kwa marupurupu wanayopewa wafanyakazi wa umma. Lakini VAT haikurejeshwa, rasmi kwa sababu ya hoja ya kubadilisha sheria ya fedha, jambo ambalo halikufanywa wakati wa kikao cha bunge cha hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.