Pata taarifa kuu
MALI-NIGER-NIGERIA-UNSC-HAKI ZA BINADAMU

G5 Sahel: UNSC yatiwa wasiwasi na ukiukwaji wa haki za binadamu

Saa chache kabla ya kutangazwa kifo cha kiongozi wa kundi la Aqmi nchini Mali, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana Ijumaa Juni 5, mjini New York, ili kuonyesha tena uungwaji wake mkono katika vita dhidi ya ugaidi inayoendeshwa na majeshi ya G5 Sahel.

Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (picha ya kumbukumbu).
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (picha ya kumbukumbu). Manuel ELIAS / UNITED NATIONS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe katika kikao hicho wamekaribisha hatua uliyopigwa na jeshi la pamoja tangu mkutano wa Pau, lakini pia wameonyesha wasiwasi wao juu ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu, vitendo vinavyotekelezwa na vikosi vya serikali, hali inayoshuhudiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Baraza la Usalama la Umoja aw Mataifa limepongeza jeshi la pamoja kwa operesheni ya kuwaangamaiza magaidi, kuwapokonbya silaha na kuwaokoa mateka waliokuwa mikononi mwa magaidi hao, na hivyo kubaini kwamba sasa muda umewadi kwa nchi tano zilizojitolea kwa wanajeshi wa kikosi hicho cha G5 Sahel kushirikiana zaidi tangu mkutano wa kilele huko Pau.

Wakati huo huo tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali imeonya juu ya kuongezeka kwa vitendo vya ukatili, hususan mauaji dhidi ya raia, na hasa dhidi ya jamii ya walio wachache ya Peul. Ripoti ya kwanza ya haki za binadamu ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA, imebaini visa 101 vinavyohusiana na mauaji ya watu waliokuwa mikononi mwa jeshi la Mali kati ya mwezi Januari na Machi, na karibu visa 30 vya mauaji vilivyotekelezwa na jeshi la Niger.

Balozi wa Niger, hata hivyo, amezitaka nchi 5 zzilizojitoliea majeshi katika kikosi cha G5 Sahel kuheshimu haki za binadamu.

"Tunatoa wito kwa jeshi hilo la pamoja kuheshimu haki za binadamu, na hasa, katika ulinzi wa raia, " amesema balozi huyo wa Niger.

Hata hivyo shinikizo hilo lilitolewa ili kuhakikisha kwamba Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet, asizungumzii tena suala hilo katika mkutano huo.

Hiyo haikuzuia baadhi ya wanadiplomasia, kama balozi wa Ubelgiji Marc Pecsteen, kukumbusha kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakuwa makini na kuchukuwa hatua za kisheria ikiwa jeshi hilo litanyooshewa kidole na kukutwa na hatia hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.