Pata taarifa kuu
DRC-ITURI-USALAMA

DRC: Jumuiya ya kimataifa yaeleza kutiwa wasiwasi na vurugu 'zisizokubalika' Ituri

Hali ya usalama na kibinadamu katika mkoa wa Ituri imezorota zaidi katika miezi ya hivi karibuni. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, zaidi ya watu 300 wameuawa na wengine karibu 200,000 wamelazimika kuoyatoroka makazi yao kutokana na machafuko yanayoendelea.

Walinda amani wa Monusco wakipiga doria kwenye mitaa ya eneo la Djugu, katika mkoa wa Ituri, unaokabiliwa na machafuko ya kikabila, Machi 13, 2020.
Walinda amani wa Monusco wakipiga doria kwenye mitaa ya eneo la Djugu, katika mkoa wa Ituri, unaokabiliwa na machafuko ya kikabila, Machi 13, 2020. SAMIR TOUNSI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mgogoro huu pia umevuka mpaka na hadi kupelekea mataifa mbalimbali kueleza kutiwa wasiwasi na hali hiyo.

Canada, Uswisi, Umoja wa Ulaya na Marekani wameelezea wasiwasi wao kuhusu machafuko yanayoendelea katika mkoa wa Ituri, Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika taarifa yao ya pamoja Ijumaa, Mei 22, Canada na Uswisi wamesisitiza juu "kutoadhibu wale wanaofanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, uhalifu wa kivita au uhalifu dhidi ya binadamu ambavyo ni makosa yasiyokubalika". Pia wamekumbusha uwepo wa mahakama kimataifa kuwaadhibu wahusika wa uhalifu huu.

Siku ya Jumatano Mei 20, Josep Borrell, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya anayehusika na sera za nje, pia alitoa wito wa "kusitishwa" kile alichokiita "vitendo vya kikatili". Mwanadiplomasia huyo wa Ulaya pia aliwakumbusha viongozi wa DRC na Tume ya Umoja wa Mataifa inayosimamia usalama na amani nchini DRC (Monusco) juu ya jukumu lao katika kusimamia na kutunza amani katika mkoa huo.

Kwa mujibu wa Josep Borrell, hali katika sehemu hii ya nchi haiwezi "kuwa mgogoro uliyosahaulika; na juhudi za kumaliza ukosefu wa usalama katika mkoa huo zinapaswa kuanza haraka iwezekanavyo. "

Kwa upande wake, Marekani imebaini kwamba "ripoti kuhusu vitendo vya kulipiza kisasi na kuundwa kwa makundi mapya ya wanamgambo ni hali inayotia wasiwasi" na inaweza "kuzidisha machafuko".

Mjini Kinshasa, Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani na mwenzake wa Ulinzi walihojiwa kwa muda wa masaa kadhaa kwenye kamati ya ulinzi ya Bunge. Wakati huo huo Serikali imetangaza kwamba hivi karibuni kuna tume ya mseto itakayozuru mkoa wa Ituri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.