Pata taarifa kuu
DRC-HRW-HAKI

DRC: HRW yalaani matumizi ya nguvu dhidi ya wafuasi wa Bundu dia Kongo

Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Right Watch limenyooshea kidole cha lawama vikosi vya usalama vya DRC katika operesheni zao dhidi ya kundi la kidini na siasa la Bundu dia Kongo huko Sangololo na jijini Kinshasa.

Vikosi vya usalama vya DRC huko Kinshasa, Februari 25, 2018.
Vikosi vya usalama vya DRC huko Kinshasa, Februari 25, 2018. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ripoti ya shirika la Human Right Watch watu wasiopungua 55 waliuawa na wengine wengi walijeruhiwa kati ya Aprili 13 na Aprili 24 katika ukandamizaji dhidi ya kundi hilo.

Wakati huo kiongozi wa Bundu dia Kongo Zacharie Badiengila, anayejulikana kwa jina maarufu Ne Muanda Nsemi, alikamatwa na kupelekwa hospitali kwa uchunguzi wa kisaikolojia. Mamlaka inashutumu wafuasi wake kwa kusababisha vurugu hizo.

"Kwa kweli polisi ilitumia nguvu kupita kiasi katika operesheni ya dhidi ya kundi la Bundu dia Kongo ("Ufalme wa Congo" katika Kikongo, BDK) kati ya Aprili 13 na 24, 2020, " shirika la Human Right Watch limebaini.

Lewis Mudge, Mkuu wa HRW barani Afrika, ameizitaka mamlaka za DRC kuanzisha uchunguzi kuhusu oparesheni mbili za polisi ambazo zilisababisha vifo vya watu wengi: "Mamlaka inatakiwa kukabiliana na vurugu za kundi la BDK, hilo liko wazi. Lakini mahakam ndi inatakiwa kutatua yote hayo, sio kujipa majukiumu ya vyombo vya sheria kwa kumwaga damu za watu. Uchunguzi wetu unaonyesha kwamba wakati wa matukio ambayo yalifanyika kati ya Aprili 13 na 24, wafuasi wa BDK walikuwa walijihami kwa fimbo. Wachache miongoni mwao walikuwa na bunduki zilizotengenezwa kienyeji. Lakini polisi walifungua moto bila kutofautisha waliyokuwa mbele yao. Kwanza, huko Sangololo ambapo polisi walizingira nyumba katikati ya usiku ambapo wafuasi kadhaa wa kundi la BDK walikuwa wamekusanyika kuandaa maandamano yao. Mamlaka inatuambia kuwa polisi walishambuliwa na wafuasi wa BDK kwa mapanga na mishale. Lakini uchunguzi wetu unaonyesha kuwa polisi walishambulia kwa risasi nyumba waliokuwemo kabla ya kuichoma kwa moto. Na siku mbili baadaye, jijini Kinshasa, wakati polisi waliingia nyumbani kwa kiongozi wa BDK kumkamata, walifyatua risasi bila kujali. Kwa hivyo huko Sangololo sawa na jijini Kinshasa, watu kadhaa waliuawa katika matukio hayo kutokana na polisi kutumia nguvu kupita kiasi. "

Shirika la Human Right Watch limetoa wito kwa mamlaka kutoa mwanga zaidi kuhusu matukio hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.