Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-USALAMA

Algeria: Serikali ya kwanza baada ya Bouteflika yatangazwa

Rais mteule wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ameteua mawaziri wa serikali mpya, wiki mbili baada ya kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi. Serikali yake ya kwanza, baada ya mtangulizi wake Abdelaziz Bouteflika.

Abdelmadjid Tebboune, wakati wa kuapishwa kwake huko Algiers, kama rais wa Algeria, Desemba 19, 2019 (picha ya kumbukumbu).
Abdelmadjid Tebboune, wakati wa kuapishwa kwake huko Algiers, kama rais wa Algeria, Desemba 19, 2019 (picha ya kumbukumbu). © RYAD KRAMDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Desemba 28, Bwana Tebboune alimteua Waziri Mkuu Abdelaziz Djerad, msomi, mwenye umri wa miaka 65, ambaye aliwahi kuhudumu kama katibu mkuu katika ofisi ya rais (1993-1995) na kisha katika Wizara ya Mambo ya nje (2001-2003), na alimtaka aunde serikali haraka iwezekanavyo.

Zaidi ya theluthi moja (11) kati ya mawaziri 28 walioteuliwa Alhamisi wiki hii waliwahi kuhudumu katika serikali iliyotangulia au katika moja ya timu za serikali kwa kipindi cha miaka 20 ya utawala wa Abdelaziz Bouteflika, ambao walilazimika kujiuzulu Aprili 2 chini ya shinikizo la maandamano makubwa yaliyoitishwa na vuguvugu la Hirak.

Hata hivyo uteuzi huo haukidhi madai ya vuguvugu la Hirak, ambalo linataka kuvunjwa kwa "mfumo" mzima uliotawala Algeria tangu uhuru wake mwaka 1962.

Rais Tebboune, 74, mwenyewe alihudumu kama waziri kwa muda mrefu katika utawala wa Abdelaziz Bouteflika, ambaye alimteua kuwa Waziri Mkuu mwezi Mei 2017 kabla ya kumtimua miezi mitatu baadaye. Alipochukua madaraka, aliahidi kutekeleza madai ya vuguvugu la Hirak, lililoundwa Februari 22, 2019 kwa kuijenga nchi katika nyanja mbalimbali.

Sabri Boukadoum kwa hivyo ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, nafasi alioshikilia katika serikali ya Noureddine Bedoui, aliyeteuliwa Machi 31 na rais Bouteflika, siku mbili kabla ya kujiuzulu.

Kamel Beldjoud, Waziri wa Nyumba katika serikali ya Bedoui, ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, nafasi ambayo alishikilia tangu kutimuliwa Salah Eddine Dahmoune Desemba 19, kwa tuhuma za kuwakandamiza na kuwachukuliwa waandamanaji wa Hirak kama "wasaliti, mamluki, mashoga ".

Belkacem Zeghmati, aliye hudumu kama Waziri wa Sheria katika serikali ya Bedoui, anaendekea kushikilia nafasi yake, sawa na Mohamed Arkab kwenye Wizara ya Nishati, Chérif Omari kwenye Wizara ya Kilimo na Youcef Belmehdi kwenye Wizara ya Maswala ya Kidini.

Tayeb Zitouni ameteuliwa kuwa Waziri wa Masuala ya Mujahideen (maveterani), nafasi anayoshikilia bila usumbufu tangu mwaka 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.