Pata taarifa kuu
TUNISIA

Raia wa Tunisia kupiga kura leo katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais

Karibu mwezi mmoja tangu kuzinduliwa kwa kura ya urais ya Tunisia na kupunguzwa kwa idadi ya wagombea kutoka 20, profesa wa sheria Kais Saied na mmiliki wa vyombo vya habari Nabil Karoui wanamenyana leo Jumapili mbele ya wapiga kura milioni saba.

Wafuasi wa mgombea Nabil Karoui wakisherehekea matokeo ya duru ya kwanza September 15 2019
Wafuasi wa mgombea Nabil Karoui wakisherehekea matokeo ya duru ya kwanza September 15 2019 REUTERS/Muhammad Hamed
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa hao wapya walifanikiwa kuwaondosha wagombea urais katika duru ya kwanza, hatua iliyodhihirisha uchungu wa wapiga kura na kutofaulu kwa maafisa kukabiliana na mkwamo wa uchumi, ukosefu mkubwa wa ajira na huduma duni za umma.

Vituo vya kupigia kura vinafunguliwa saa 8:00 asubuhi (0700 GMT) kwa ajili ya duru ya pili na ya mwisho ya uchaguzi huo ambapo saa 12 za kupiga kura zitaamua kiongozi wa pili wa nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

Zoezi la kupiga kura linatarajiwa kufungwa Jumapili jioni.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.