Pata taarifa kuu
MUGABE-ZIMBABWE-SIASA-MAZISHI

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe azikwa kijijini

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe alizikwa siku ya Jumamosi  katika kijiji alichozaliwa Magharibi mwa jiji kuu Harare, na kuhimitisha mvutano kati ya serikali na familia yake ni wapi kiongozi huyo wa zamani aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 37, angepumzishwa.

Wanajeshi wakiwa wamebeba mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe
Wanajeshi wakiwa wamebeba mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Mazishi hayo yalihudhuriwa tu na watu wa karibu wa familia ya Mugabe, huku mkewe Grace na watoto wakionekana kuzingira jeneza lake.

Ripoti zinasema kuwa, familia ya Mugabe aliyefariki dunia mapema mwezi Septemba akiwa na umri wa miaka 95 nchini Singapore, iliamua azikwe katika kijiji alichozaliwa cha Kutama.

Familia yake ambayo ilikuwa imekubali kuwa Mugabe azikwe kwenye makaburi ya mashujaa baada ya kuelewana na serikali, hata hivyo, ilibadilisha msimamo wake.

Waziri wa Habari nchini humo Nick Mangwana katika taarifa yake wiki hii amesema, serikali ilikubali na kuheshimu ombi la serikali kuhusu ni wapi Mugabe azikwe.

Mwezi huu kulikuwa na ibada ya kumbumbuka Mugabe iliyofanyika jijini Harare na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.