Pata taarifa kuu
MISRI-SIASA-USALAMA

Polisi ya Misri yawashikilia watu zaidi ya 500

Watu zaidi ya 500 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali nchini Misri kwa kipindi cha siku kadhaa zilizopita, wakati wa maandamano dhidi ya rais wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Sisi.

Mamia ya waandamanaji waliokusanyika katika mji wa Cairo Jumamosi, Septemba 21, 2019.
Mamia ya waandamanaji waliokusanyika katika mji wa Cairo Jumamosi, Septemba 21, 2019. REUTERS/Mohamed Abd El Ghany
Matangazo ya kibiashara

Watetezi wa haki za binandamu wametoa takwimu hizo kutokana na maandamano yaliyofanyoka siku ya Ijumaa na Jumamosi iliyopita jijini Cairo na maeneo mengine ya nchi hiyo.

Miongoni mwa watu waliokamatwa ni mwanaharakati maarufu Mahienour el-Massry aliwahi kushinda tuzo ya Kimataifa.

Maafisa wa usalama wanamshtumu el Massry kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi lakini pia kuhusika na uchapishaji wa habari za uongo.

Waandamanaji nchini Misri wakati wa maandamano hayo, walikuwa wanalalamikia kuendelea kuteswa kwa wapinzani wa rais el Sisi, na kuzuiwa kushiriki katika maandamano dhidi ya utawala wake.

Maandamano nchini Misri, yamepigwa marufuku nchini Misri tangu mwaka 2013 wakati rais wa zamani Mohammed Morsi alipoondolewa madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.