Mwanasheria maarufu akamatwa nchini Misri
Malaka nchini Misri zinamshikilia Mwanasheria Mshindi wa tuzo ya Haki za Binadamu baada ya kufuatilia uchunguzi wa kukamatwa kwa waandamaji waliokuwa wakimpinga Rais wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Sisi.
Imechapishwa:
Tarek al-Awadi Mwanasheria wa Mahienour El-Massry anasema mwanasheria huyu alikamatwa muda mfupi tu baada ya kuondoka katika ofisi ya mwendesha mashataka wa serikali jijini Cairo alipokuwa akifuatiliwa kukamatwa kwa waandamaji.
Mamia ya Wamisri waliingia Mitaani jijini Cairo pamoja na miji mingine wakishinikiza kuondoka madarakani kwa Rais al-Sisi.
Kwa Mujibu wa kituo kinachoshughulikia haki za kiuchumi na kijamii nchini humo Watu 365 wamekamatwa kutokana na Maaandamano hayo
Mwezi wa Decemba 2013, kufuatia Jeshi kumpindua rais wa zamani Mohamed Morsi baada ya maandamano ya kushinikiza ang'atuke Madarakani Bi El-Massry alikamatwa na kufungwa Jela hadi Septemba 2014 kwa kosa la kushiriki maandamano bila kibali akiwa Gerezani ndipo alipata tuzo ya haki za binadamu