Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UGAIDI-USALAMA

Watu 29 waangamia katika mashambulio mawili Burkina Faso

Watu 29 wamuawa Kaskazini mwa Burkina Faso katika mashambulio mawili. Lori la uchukuzi limekanyaga bomu la kutegwa ardhini lililotengenezwa kienyeji na kusababisha vifo vya watu 15.

Operesheni ya kijeshi inaendelea kati ya maeneo ya Guendbila na Baaalogho, kwa mujibu wa serikali (picha ya kumbukumbu).
Operesheni ya kijeshi inaendelea kati ya maeneo ya Guendbila na Baaalogho, kwa mujibu wa serikali (picha ya kumbukumbu). AFP PHOTO/ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo watu wenye silaha wameshambulia msafara wa chakula amabacho kilikuwa kinasafirishwa kwa wakimbizi wa ndani katika wilaya ya Kelbo.

Mashambulio yote mawili yalitokea katika mkoa wa Kaskazini. Lori la kubeba mizigo, ambalo pia lilikuwa na abiria, lilikanyaga kifaa cha kulipuka. Shambulio hilo lilitokea saa sita mchana, kati ya maeneo ya Guendbila na Baaalogho, kulingana na chanzo cha usalama.

Lori liliharibika sana, kulingana na mashahidi. miongoni mwa wahanga ni pamoja na wanawake na watoto.

Asakari wengi wametumwa katika eneo la tukio na operesheni za kijeshi zinaendelea kwa mujibu wa serikali.

Shambulio la pili lililenga msafara wa chakula kwa watu wa Kelbo na maeneo jirani, katika mkoa wa Kaskazini. Chakula kilipelekwa na vikosi vya ulinzi na usalama hadi wilayani Dablo. "Kutokana na hali mbaya ya barabara, msaada huo wa chakula, ulihamishwa na kusafirishwa kwa kutumia pikipiki za matairi matatu," chanzo cha usalama kimesema. Pikipiki hizi ndizo zilishambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana kati ya Dablo na Kelbo.

Kwa mujibu wa serikali, shambulio hili lilitekelezwa na magaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.