Pata taarifa kuu

Jaribio la mapindizi Burkina Faso: Wengi waridhishwa na hatua ya mahakama, washtumiwa walaani

Wadau mbalimbali nchini Burkinafaso wameridhishwa na hukumu iliotolewa Jumatatu wiki hii na hakama ya kijeshi kwa majenerali Gilbert Diendere aliehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela na Djibril Bassole aliehukumiwa kufungo cha miaka 10 jela.

Vinara wa jaribio la mapinduzi Burkina Faso mwaka 2015, Jenerali Gilbert Diendéré (kushoto) na Djibrill Bassolé.
Vinara wa jaribio la mapinduzi Burkina Faso mwaka 2015, Jenerali Gilbert Diendéré (kushoto) na Djibrill Bassolé. AFP/Ahmed Ouoba
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa zamani wa shirika la upelelezi la Burkina Faso, Jenerali Gilbert Diendere amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kupatikana na hatia ya kufanya mauaji na kutishia usalama wa taifa.

Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Djibril Bassole ambaye analaumiwa kuwa ndiye aliyekuwa mratibu mkuu wa jaribio hilo, amehukumiwa kifungo cha miaka 10.

Wakili wa upande wa serikali amesema hatua hiyo ni muhimu na ni ushindi kwa wananchi wa Burkina Faso.

Hata hivyo Mathieu Somé, wakili mtetezi wa jenerali Gilbert Diendere aliehukumiwa kifungo cha miaka 20 amesema kesi hiyo ni ya kisiasa.

Viongozi wa asasi za kiraia, jamaa za wahasiriwa na waliojeruhiwa wanasubiri hatua ya pili ya kesi hiyo ambayo itaangalia kuhusu fidia ya waathirika na waliojeruhiwa.

Jaribio hilo la mapinduzi lililoendelea kwa kipindi cha wiki moja lilishindwa lakini watu 14 waliuawa na wengine zaidi ya 250 kujeruhiwa wakijaribu kukabiliana na kundi la wafanyamapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.