Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-MAKUBALIANO

Sudani yasherehekea makubaliano ya kihistoria, uteuzi wa Baraza Kuu wacheleweshwa

Sudanii inaendelea kusherehekea makubaliano ya kihistoria yaliyosainiwa na viongozi wa kijeshi na wale wa maandamano kwa lengo kuundwa kwa taasisi za mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Viongozi wa maandamano baada ya kusaini tamko la katiba na wanajeshi Agosti 4, 2019 Khartoum.
Viongozi wa maandamano baada ya kusaini tamko la katiba na wanajeshi Agosti 4, 2019 Khartoum. ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo uteuzi uliotarajiwa wa Baraza Kuu la uongozi wa nchi litakalosimamia taasisi hizo za mpito umeahirishwa hadi leo Jumatatu.

Raia nchini Sudan walidhihirisha furaha yao jana Jumapili, siku moja baada ya kusainiwa kwa mkataba wa taasisi za mpito kwa kipindi cha miezi 39 kati ya viongozi wa jeshi na viongozi wa maandamano.

Taasisi hizo za mpito zitasimamiwa na "Baraza Kuu" linajumuisha wajumbe 11 - raia sita na askari watano.

Tangazo la kuundwa kwa Baraza Kuu halikutokelewa tena na jioni. Kulingana na vyanzo vya upinzani, wajumbe watano tu kati ya kumi na moja ndio wameteuliwa mpaka sasa, na zoezi hilo linatarajiwa kufanyika leo Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.