Pata taarifa kuu
LIBYA-AU-UN-USALAMA

EU yatoa wito wa kusitishwa mapigano Libya na kuunga mkono mjumbe wa UN

Umoja wa Mataifa umetoa tena wito kwa pande zinazokinana nchini Libya kusitisha mapigano na kudumisha amani, huku ukionyesha uungwaji wake mkono kwa Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo, anayeshtumiwa na Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj kwamba "hana ukweli wowote".

Mkuu wa sera za kigeni za Umoja wa Ulaya Federic Mogherini.
Mkuu wa sera za kigeni za Umoja wa Ulaya Federic Mogherini. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

"Umoja wa Ulaya na wanachama wake wanakaribisha pendekezo la kusitishswa kwa mapigano lililotolewa na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ghassan Salamé, kwenye hafla ya Eid al-Adha (Sikukuu ya kuchinja wanyama halali), ambayo ni hatua muhimu katika mwelekeo huo, "Mkuu wa sera za kigeni za Umoja wa Ulaya Federic Mogherini amesema, katika taarifa kwa niaba ya Umoja wa Ulaya.

"Umoja wa Ulaya unaunga mkono kikamilifu ombi la Mwakilishi Maalum kwa hatua tatu zinazolenga kufufua mazungumzo ya kisiasa na hasa kutekeleza mpango huo bwa kusitishwa kwa mapigano ," Mogherini ameongeza.

"Mashambulio ya kinyama kwenye maeneo yenye wakazi wengi yanaweza kuwa uhalifu wa kivita na wale wanaokiuka sheria za kimataifa za binadamu wanapaswa kufikishwa mbele ya mahakama na wawajibishwe," Mogherini ameonya.

"Umoja wa Ulaya na wanachama wake wametoa wito kwa wanachama wote wa Umoja wa Mataifa kuheshimu vikwazo vya silaha dhidi ya Libya" na umezitaka pande zote husika katika mzozo nchini Libya "kujitenga, hadharani na magaidi pamoja na wahalifu wanaoshiriki vita na wale wanaoshtumiwa kutekeleza uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na wale waliowekwa kwenye orodha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.