Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Moise Katumbi: Mei 20, nitarudi Lubumbashi kwa ndege

Kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa urais Desemba 30, kiongozi wa upinzani nchini DRC, Moïse Katumbi Chapwe, amevunja ukimya kuhusu kuendelea kusalia uhamishoni.

Moïse Katumbi wakati katika mahojiano na RFI na France24, Mei 6, 2019.
Moïse Katumbi wakati katika mahojiano na RFI na France24, Mei 6, 2019. © RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Akihojiwa na wenzetu Christophe Boisbouvier wa RFI na Marc Perelman wa France 24, mratibu wa muungano wa upinzani Lamuka ametangaza kwamba baada ya miaka mitatu akiwa uhamishoni, anatarajia kurudi kwa ndege Lubumbashi Mei 20.

Moise Katumbi , mfanyabiashara tajiri na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga , alizuiliwa kuingia nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kushitakiwa kwa makosa dhidi ya usalama wa taifa. Katumbi mwenye umri wa miaka 53, anaishi uhamishoni nchini Ubelgiji tangu Mei 2016 baada ya kutofautiana na rais Joseph Kabila, ambaye ameitawala DRC kwa miaka 17.

Hivi karibuni vyombo vya sheria vya DRC vilimsafisha Moise Katumbi kwa makosa mawili yaliyokuwa yakimkabili katika kesi ya madai ya udanganyifu wa mali. Pia alikuwa anashutumiwa kwa kukodi mamluki na kuwa na pasi ya kusafiria ya italia, ambapo sheria za Congo haziruhusu mtu kuwa na uraia pacha wa mataifa mawili.

Moise Katumbi amepongeza vyombo vya sheria vya DRC kwa hatua hiyo na kusema ana furaha ya kurejea nchini.

Kiongozi huyo wa upinzani alikataliwa kuingia DRC kupitia mpaka na Zambia wakati alipojaribu kurejea kutoka uhamishoni ili kuwasilisha fomu yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwezi Desemba.

Katumbi alikuwa anatakabiliwa na kukamatwa baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela wakati akiwa hayupo mahakamani mwezi Juni 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.