Pata taarifa kuu
EBOLA-DRCONGO

Miezi 9 tangu kuzuka kwa Ebola,vifo mia tisa mashariki mwa DRC

Ugonjwa wa Ebola umesababisha vifo vya watu 900 tangu mwezi Agost mwaka jana katika eneo la mashariki mwa DRC ambako ukosefu wa usalama na uasi vimesababisha ugumu katika mapambano kwa mujibu wa mamlaka za afya nchini humo.

Mtoa huduma ya afya akimpatia raia chanjo ya Ebola mashariki mwa DRC
Mtoa huduma ya afya akimpatia raia chanjo ya Ebola mashariki mwa DRC REUTERS/Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwanzo wa mlipuko huo jumla ya visa 1396 vilikusanywa ikiwemo 1330 vilivyothibitika na vinavyochunguzwa 66.

Jumla ya vifo 900 vimeripotiwa hadi kufikia April 25 kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya nchini DRC.

Wakati Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ikipambana na mlipuko wa pili mkubwa wa ugonjwa wa Ebola, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP lilitahadharisha hivi karibuni kuwa rasilimali zinazohitajika kusaidia shughuli zake, haziendani na kasi ya ongezeko la hivi karibuni la maambukizi na uwepo wa hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo ndani ya DRC na katika nchi za jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.