Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAJANGA ASILI

Nigeria: Nane wauawa baada ya jengo moja kuporomoka Lagos

Jengo la ghorofa tatu limeporomoka na kuua watu wanane katika eneo la Mercy Street, Ita-Faaji Lagos Island, tukio ambalo limetokea leo Jumatano asubuhi. Shule ya wanafunzi zaidi ya 100 limekuwa kwenye ghorofa ya tatu, vyumba vya makazi kwenye ghorofa ya pili na maduka kwenye sehemu ya chini.

Waokoaji waendelea na shughuli ya kuondoa udongo na mawe kuwaokoa watu waliokwama chini ya vifusi vya jengo lililoanguka Lagos Island.
Waokoaji waendelea na shughuli ya kuondoa udongo na mawe kuwaokoa watu waliokwama chini ya vifusi vya jengo lililoanguka Lagos Island. Ahmed Abba/RFI
Matangazo ya kibiashara

Afisa wa idara ya hali ya dharura katika eneo hilo Ike Okwonkwo ameiambia BBC kwamba wanafunzi 8 wamefariki dunia na wengine 40 wameokolewa mpaka sasa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, na mkuu wa idhaa ya kiswahili ya RFI Robert Minangoy ambaye yuko jijini Lagos amesema watoto 10 ndio wamekwama chini ya vifusi.

Shughuli za uokoaji zinaendelea sasa, na watu wengi wameokolewa kutoka chini ya vifusi vya jengo hilo kwa jitihada za pamoja za idara inayokabiliana na majanga kutoka jimbo la Lagos (LASEMA) na idara nyingine.

Shughuli hizo zinaratibiwa na Mkurugenzi Mkuu wa LASEMA, Bw Adesina Tiamiyu, baada ya kupelekwa vifaa muhimu vya uokoaji.

Kwa mujibu wa BBC, ikinukuu mkaazi mmoja, serikali ya jimbo la Lagos iliamuru jengo hilo libomolewa tangu mwaka 2018 lakini watu wanaoishi katika jengo hilo walikataa kuondoka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.