Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-UCHAGUZI

Algeria yaendelea kukumbwa na maandamano

Wananchi wa Algeria wanatarajia kumiminika mitaani leo Ijumaa katika miji mikubwa ya nchi hiyo kupinga rais Abdelaziz Bouteflika kuwania muhula wa tano. Kama Ijumaa ya wiki iliyopita, wito wa kuwataka wananchi kuandamana umeendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Maandamano ya wanafunzi wa Algeria jijini Algiers, Februari 26, 2019.
Maandamano ya wanafunzi wa Algeria jijini Algiers, Februari 26, 2019. © STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya ambayo yalianzishwa hasa na vijana, hivi karibuni vyama karibu vyote vya upzinani vilijunga na vijana hao na kupinga Abdelaziz Bouteflika kuwania tena muhula wa tano katika uchaguzi ujao.

Vijana wa Algeria ambao wanapinga muhula wa tano wana imani ya kukusanya watu zaidi kuliko Ijumaa ya wiki iliyopita. Tunataka wananchi wote waelewe kuwa nchi sio ya mtu mmoja pekee, watu wote wana haki ya kuongoza Algeria kupitia uchaguzi. Waandamanaji wanataka Abdelaziz apishe wengine kwenye uongozi wa nchi na kumalizika kwa utawala wake ambao wanaona kuwa rushwa imekithiri, na ni utawala wa kiimla na ameshindw kufufua uchumi.

Tangu wiki iliyopita, karibu vyama vyote vya upinzani vimejiunga na waandamanaji. Wanafunzi pia wamehamasishwa wiki hii, hata waandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari vya serikali, ili kupinga udhibiti na shinikizo wanazozipata katika kazi yao.

Mapema wiki hii Waziri Mkuu wa Algeria alitangaza kuwa rais Bouteflika atapeleka fomu yake ya kuwania katika uchaguzi ujao Jumapili Machi 3, tarehe ya mwisho kwa wagombea waliochelewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.