Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-UCHAGUZI

Uchaguzi wa urais Algeria kufanyika Aprili 18

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ametangaza kuwa Uchaguzi wa urais utafanyika nchini humo tarehe 18 mwezi Aprili mwaka huu.

Kwa kipindi cha miaka sita, Bouteflika hajawahi kulihotubia taifa kutokana na kudhoofika kiafya.
Kwa kipindi cha miaka sita, Bouteflika hajawahi kulihotubia taifa kutokana na kudhoofika kiafya. REUTERS/Ramzi Boudina
Matangazo ya kibiashara

Licha ya rais Bouteflika kutoa tangazo hilo, haijafahamika iwapo kiongozi huyo mwenye miaka 81, aliyeanza kuongoza nchi hiyo tangu mwaka 1999, atawania wadhifa huo kwa muhula wa tano.

Miaka ya hivi, karibuni, kiongozi huyo ambaye ameendelea kusalia kwenue baiskeli ya magurudumu tangu mwaka 2013, amekuwa akikosolewa na wapinzani na wakuu wa jeshi iwapo ataamua kuwania tena.

Djamel Ould Abbes, mwanzilishi wa chama tawala National Liberation Front (FLN), alifutwa kazi mwezi Novemba mwaka uliopita, baada ya kutangaza kuwa chama hicho kitamsimamisha rais Bouteflika kuwania tena urais.

Kwa kipindi cha miaka sita, Bouteflika hajawahi kulihotubia taifa kutokana na kudhoofika kiafya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.