Pata taarifa kuu
DRC-NAMIBIA-USHIRIKIANO

Rais mpya wa DRC azuru Namibia

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ameanza ziara ya siku mbili nchini Namibia ambapo hapo jana amekutana na mwenyeji wake rais wa Namibia Hage G. Geingob, kwa mazungumzo yanayolenga kuboresha mahusiano ya kibiashara kati ya mataifa yao mawili.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi katika kikao cha Umoja wa Afrika (AU) Februari 10, 2019.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi katika kikao cha Umoja wa Afrika (AU) Februari 10, 2019. SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya rais jijini Windoek huko Namibia ni kuwa rais Felix Tshisekedi wa DRC na mwenzake wa Namibia Hage G. Geingob wamejadili kuhusu mahusiano ya kibiashara ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuwapata wawekezaji zaidi hususan katika sekta ya madini, DRC ikiwa ni nchi tajiri katika uzalishaji wa madini katika ukanda wa Afrika ya kati.

Chanzo hicho, kimeenda mbali na kuelezea kuwa rais wa DRC ataitamatisha ziara yake hiyo na kurejea Kinshasa Jumatano wiki hii.
Rais Geingob wa Namibia amefahamisha kupitia akaunti yake ya Twitter kuwa amepata matumaini mapya ya kuona maendeleo ya kiuchumi ya SADC na bara la Afrika kwa ujumla, kufwatia uwezo wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Rais huyo wa Namibia pia ameongeza kuwa ziara ya rais Tshisekedi nchini Namibia imedhirihirisha hatua muhimu ambayo imepigwa mpaka sasa katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati nchi hizi mbili.

Imekuwa ni ziara ya tatu ya rais Tshisekedi nje ya nchi tangu achukuwe hatamu ya uongozi wa taifa hilo Januari 24 mwaka huu, baada ya kushiriki mkutano wa viongozi wa mataifa ya Afrika uliofanyika Addis Ababa Ethiopia Februari 10 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.