Pata taarifa kuu
DRC-UN-AFYA-TUZO YA NOBEL

Tuzo ya Nobel: Dk Mukwege aomba Umoja wa Mataifa kulinda raia DRC

Siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuu nchi DRC, Dk maarufu anayeshughulikia upasuaji wa magonjwa ya wanawake nchini DRC Denis Mukwege amesema anashangazwa na kushindwa kwa mkakati wa jumuiya ya kimataifa na uhalifu unaoendelea katika nchi yake.

Dk Denis Mukwege, anayeshughulikia upasuaji wa magonjwa ya wanawake nchini DRC.
Dk Denis Mukwege, anayeshughulikia upasuaji wa magonjwa ya wanawake nchini DRC. SAFIN HAMED / AFP
Matangazo ya kibiashara

Dk Denis Mukwege, mwenye umri wa miaka 58 anatarajia leo Jumatatu kupata tuzo ya amani ya Nobel huko Oslo.

Denis Mukwege ambaye licha ya vitisho kwa maisha yake amejizatiti kuwasaidia wanawake wahanga wa ubakaji katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Daktari huyo ambaye hasa anashughulikia upasuaji wa magonjwa ya wanawake mara kwa mara amekuwa akikemea ukatili wa ngono dhidi ya wanawake ambao umekuwa ukitumika kama silaha ya vita.

Kwa Tuzo ya Olof Palme aliyotunukiwa mwaka 2009 anasema kwake yeye hicho ni kitu kidogo sana lakini alijiambia mwenyewe kwamba itakuwa vyema kuendelea na kazi hiyo ya kuwasaidia watu.

Mukwege alisomea udaktari katika nchi jirani ya Burundi na alifanya kazi katika hospitali ya mji mdogo wa Lemera katika eneo la vijijini mkoani Kivu Kusini.

Dk Mukwege anasema alifadhaishwa na idadi ya wanawake wanaofariki duni kila kukicha katika kijiji hicho kwa sababu za uzazi.

"Hilo ndilo lilinichochea nisomee zaidi matibabu ya wanawake, nilipokwenda Ufaransa kusomea elimu juu ya magonjwa ya kike na ukunga. " amesema Bw Mukwege.

Hata hivyo Dk denis Mukwege ameanzisha mipango ya msaada wa kisaikolojia na wa kisheria kwa wahanga wa ubakaji.

Mukwege anataka kushughulikia mzizi wa tatizo hilo na kukemea vita vya kiuchumi vinavyoshamiri nchini Congo ambapo waasi na serikali wanagombania udhibiti wa mapato ya mali asili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.