Pata taarifa kuu
NIGERIA-SIASA

Buhari anadi sera yake katika kampeni za kisiasa Nigeria

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameanza kampeni za kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Februari mwaka 2019, licha ya hali yake ya afya kudorora katika miezi ya hivi karibuni.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, hivi karibuni alitangaza kwamba atawania katika uchaguzi wa urais ujao kwa muhula wa pili.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, hivi karibuni alitangaza kwamba atawania katika uchaguzi wa urais ujao kwa muhula wa pili. Daniel Leal-Olivas/ Reuters/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Buhari mwenye umri wa miaka 75, anawania muhula wa pili wa miaka minne, kuongoza taifa hilo la Afrika Magharibi lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, huku ujumbe wake wa kampeni ukiwa ni kuendeleza vita dhidi ya ufisadi.

Rais huyo amewaambia wafuasi wake jijini Abuja, kuwa kwa muda wa miaka minne ambayo amekuwa madarakani, ametekeleza ahadi ya kuimarisha usalama lakini pia kupambana na rushwa.

Hata hivyo, amekiri kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya, kuhakikisha kuwa magaidi wa Boko Haram wanashindwa na uchumi unaimarishwa.

Buhari anapambana na aliyekuwa Makamu wa rais Atiku Abubakar, anayepeperusha bendera ya chama kikuu cha upinzani cha PDP, huku wachambuzi wa siasa wakisema ushindani utakuwa ni mkali.

Wagombe 78 kutoka vyama 91, wanawania urais nchini Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.