Pata taarifa kuu
BOKO HARAM-NIGERIA-UGAIDI

Boko Haram wawauwa watu wawili na kushambulia kijiji Kaskazini mwa Nigeria

Kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram wameua watu wawili baada ya kushambulia kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa nchi ya Nigeria, kijiji kilichokuwa jirani kabisa na mji wa Chibok. 

Kiongozi wa Boko Haram  Abubakar Shekau
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau © AFP PHOTO / BOKO HARAM
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa polisi wa eneo la Mifah, wamethibitisha kutekelezwa kwa shambulio hilo na wanaodhaniwa kuwa ni wapiganaji wa Boko Haram wanaoongozwa na Abubakar Shekau, ambapo hivi karibuni wameendelea kutekeleza mashambilizi mfululizo.

Taarifa zinasema kuwa wapiganaji hao mbali na kuua raia, walichoma moto nyumba za wananchi na kusababisha mamia ya raia wengine kukimbilia kwenye mji wa Chibok kukwepa kuuawa.

Shambulio hili linaripotiwa ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu wapiganaji hao watekeleze shambulio jingine kaskazini mwa jimbo la Borno ambako watu zaidi ya 10 waliuawa.

Jumla ya watu elfu 27 wameuawa tangu kundi hilo lianze kutekeleza mashambulizi miaka 9 iliyopita.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.