Pata taarifa kuu
MOROCCO-VATICAN-PAPA-USHIRIKIANO

Papa Francis kuzuru Morocco mwezi Machi

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis anatarajiwa kuzuru nchi ya Morocco ifikapo mwezi Machi mwaka 2019. Vatican imethibitisha ziara hii na imebaini kwamba itafanyika kuanzia Machi 30 hadi 31.

Papa Francis, Vatican Oktoba 10, 2018.
Papa Francis, Vatican Oktoba 10, 2018. Alberto PIZZOLI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mfalme Mohammed VI pamoja na Maaskofu Katoliki nchini Morocco, wamemwalika Baba Mtakatifu Francisko kutembelea nchi yao kuanzia tarehe 30-31 Machi 2019. Katika ziara hii, Papa Francis anatarajiwa kutembelea mji wa Rabar na Casablanca.

Ratiba ya ziara hii inatarajiwa kutolewa hivi karibuni kwa mujibu wa Dr. Greg Burke, msemaji mkuu wa Vatican.

Papa Francis anataka kuendeleza majadiliano ya kidini na waamini wa dini mbali mbali duniani, ili kujenga na kudumisha umoja, upendo, haki na mshikamano wa dhati na kwamba, tofauti mbali mbali zisiwe ni chanzo cha vurugu na mitafaruku ya kijamii na kidini, Dr. Greg Burke amesema.

Papa Francis ni kiongozi wa pili wa kanisa Katoliki kuzuru Morocco baada ya Papa John Paul II kuzuru nchi hiyo mnamo mwaka 1985 wakati wa utawala wa Hassan II.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.