Pata taarifa kuu
TUZO-NOBEL-2018-MUKWEGE-MURAD

Daktari Mukwege na Mwanaharakati Murad washinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2018

Daktari kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Denis Mukwege na mwanaharakati Nadia Murad kutoka Iraq ndio washindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2018. 

Washindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2018 Nadia Muradna kutoka DRC  Denis Mukwege
Washindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2018 Nadia Muradna kutoka DRC Denis Mukwege REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wametangazwa washindi na Kamati ya Nobel yenye makao yake jijini Oslo nchini Norway kutokana na harakati zao za kupinga matumizi ya ngono kama silaha katika maeneo yenye vita.

Murad aliwahi kutekwa na kundi la Islamic State kwa muda wa miezi mitatu na kutumikishwa kingono kabla ya kufanikiwa kutoroka na kuanza harakati hizo.

Naye Daktari Mukwege, kwa muda mrefu sasa amekuwa katika mstari wa mbele kuwasadia wanawake na wasichana wanaobakwa katika maeneo yenye vita Mashariki mwa DRC.

Daktari huyo ambaye ni mtaalam wa magonjwa ya wanawake, anamiliki Hospitali aliyoipa jina Panzi, mjini Bukavu.

Mukwege amesema alikuwa katika chumba cha upasuaji aliposikia Habari njema kuwa alikuwa amepewa tuzo hiyo, baada ya watu kuanza kuimba kwa furaha nje ya Hospitali yake.

“Nilikuwa katika chumba cha upasuaji niliposikia watu wanapiga kelele na nilipouliza, nikaambiwa kuwa nimeshinda tuzo hii,” ameliambia Gazeti la Noray VG.

“Nilijawa na hisia nyingi sana, niliposikia watu wanalia baada ya kusikia tangazo hilo,” aliongeza.

Daktari huyo mwenye umri wa miaka 63, amekuwa akipata umaarufu mkubwa kwa kutoa huduma anayotoa katika eneo hilo ambalo kwa muda mrefu halijashuhudia amani.

Serikali ya Kinshasa imepongeza Mukwege, lakini ikamkosoa kuwa pamoja na kufanya kazi nzuri, anaingiza siasa katika kazi yake.

“Serikali inampongeza sana Daktari Mukwege kwa kazi muhimu anayofanya licha ya tofauti zetu,” alisema msemaji wa serikali Lambert Mende.

Mukwege ambaye kwa jina lingine anaitwa, muujiza, amekuwa mkosoaji mkubwa wa rais Kabila, akimtaka kutowania urais kwa muhula wa tatu.

Felix Tshisekedi, mwanasiasa wa upinzani naye pamoja na pongezi amesema, Mukwege amemfanya kujivunia kuwa raia wa DRC.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.