Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-UCHAGUZI-HAKI

Upinzani waomba kufutwa kwa uchaguzi wa rais Mnangagwa

Upinzani nchini Zimbabwe umeomba Mahakama ya Katiba kufuta uchaguzi wa rais anayemaliza muda wake Emmerson Mnangagwa, ukishtumu serikali yake kuhusika katika wizi wa kura. Upinzani pia umeshtumu tume ya uchaguzi kwamba ilihusika katika wizi huo.

Mawakili wanaomuwakilisha kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Chnge (MDC) Nelson Chamisa wakiwasili kwenye mahakama ili kupinga ushindi wa rais Emmerson Mnangagwa huko Harare Agosti 22, 2018.
Mawakili wanaomuwakilisha kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Chnge (MDC) Nelson Chamisa wakiwasili kwenye mahakama ili kupinga ushindi wa rais Emmerson Mnangagwa huko Harare Agosti 22, 2018. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mbele ya majaji tisa wa mahakama ya juu zaidi nchini Zimbabwe, wanasheria wa Movement for Democratic Change (MDC) kwa muda mrefu wametaja makosa ambayo, wanaona kuwa yalihusika kuvuruga uchaguzi wa Julai 30, uchaguzi wa kwanza tangu Robert Mugabe kutimuliwa madarakani miezi nane iliyopita.

"Hili ni jaribio kubwa la wizi, sisi tunakabiliana na jaribio la kutumiwa vibaya," amesema mmoja wao, Thabani Mpofu, mbele ya mahakama.

Bw Mnangagwa ambaye alipeperusha bendera ya chama cha Zanu-PF katika uchaguzi wa urais alishinda kwa 50.8% ya kura dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa, ambaye alipata 44.3% ya kura.

"Tuliorodhesha vituo 16 vya kupigia kura ambapo matokeo yanafanana, sauti za ya kura zinazofanana kwa Chamisa, sauti za kura zinazofanana kwa Mnangagwa," amebainisha Bw Mpofu, "ni kana kwamba mtoto alikuwa akifurahishwa kucheza na hesabu ".

Mahakama inaweza kuthibitisha matokeo, kutoidhinisha na kupiga kura upya au kuagiza kurudiwa kuhesabu upya kwa sauti za kura.

Kukata rufaa kwa chama cha MDC tayari kumesababisha kuahirishwa kwa sherehe ya kutawazwa rais Mnangagwa, ambayo awali iliyopangwa kufanyika Agosti 12. Ikiwa Mahakama itathibitisha ushindi wake, sherehe itafanyika ndani ya saa arobaini na nane baada ya uamuzi wa Mahakama ya Katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.