Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Upinzani wajaribu kuungana kabla ya uchaguzi wa urais DRC

Umoja wa Afrika na Ulaya, umempongeza rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila, kwa kumteua mrithi wake kuwania urais wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Desemba.

Vital Kamerhe baada ya kuwasilisha fomu ya kuwania katika uchaguzi kwenye Tume ya Uchaguzi (CENI) huko Kinshasa, DRC, Agosti 6, 2018 (picha ya kumbukumbu).
Vital Kamerhe baada ya kuwasilisha fomu ya kuwania katika uchaguzi kwenye Tume ya Uchaguzi (CENI) huko Kinshasa, DRC, Agosti 6, 2018 (picha ya kumbukumbu). Patient Ligodi/RFI
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, AU na EU zinataka rais Kabila kwenda mbali zaidi na kuhakikisha kuwa makubaliano ya kisiasa ya mwaka 2016 yanatekelezwa kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa, kuwashirikisha wanasiasa wote katika uchaguzi huu na kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unakuwa huru na haki.

Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa licha ya sasa kuwa wazi kuwa Kabila hatawania tena baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 17, bado kuna hali ya wasiwasi kuhusu mustakabali wa uchaguzi huo.

Mbali na hilo, ripoti zinasema kuwa wanasiasa wa upinzani walikutana Alhamisi wiki hii kuona namna ya kumteua mgombea mmoja na kushinikiza kurejea kwa Moise Katumbi Chapwe kuelekea Uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.