Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Kingozi wa juu wa upinzani Tendai Biti akamatwa Zimbabwe

Kiongozi wa juu wa upinzani nchini Zimbabwe Tendai Biti amekamatwa Jumatano wiki hii katika mpaka wa Zambia wakati ambapo chama chake kinaendelea kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais, amebaini mwanasheria wake.

Tendai Biti, moja kati ya viongozi wa juu wa upinzani, na waziri wa zamani wa Fedha wa Serikali ya Umoja wa kitaifa (mnamo mwaka 2009-2013).
Tendai Biti, moja kati ya viongozi wa juu wa upinzani, na waziri wa zamani wa Fedha wa Serikali ya Umoja wa kitaifa (mnamo mwaka 2009-2013). Reuters/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe (ZEC) ilimtangaza Emmerson Mnangagwa, kuwa alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 50.8.

"Amekamatwa kwenye mpaka wa Zambia," Nqobizitha Millo amesema, akiongeza kwenye ujumbe wa simu (SMS) kwamba waziri huyo wa zamani alikuwa akitafuta "hifadhi" ya ukimbizi katika nchi jirani ya Zambia.

Mmoja kati ya viongozi wa juu wa upinzani, na waziri wa zamani wa Fedha wa Serikali ya Umoja wa kitaifa (mnamo mwaka 2009-2013), Biti anatafutwa na mahakamani, wbaada ya kushtumiwa kuchochea vurugu, kwa mujibu wa gazeti la The Chronicle, linalounga mkono serikali.

Bw Biti alitangaza kabla ya kutangazwa rasmi matokeo ya uchaguzi na Tume ya Uchaguzi kwamba Nelson Chamisa, mgombea wa chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) alishinda uchaguzi, huku akiishtumu Tume ya Uchaguzi kwa kutangaza matokeo tofauti.

Tume ya uchaguzi ilimtangaza Bw Mnangagwa, aliyekuwa mshirika wa karibu wa Robert Mugabe, aliyetimuliwa madarakani na jeshi mnamo mwezi Novemba baada ya miaka 37 ya kuitawala nchi hiyo, mshindi wa uchaguzi huo kwa asilimia 50.8.

Hatua ya vikosi vya usalama na ulinzi kuvunja maandamano ya upinzani ilisababisha watu sita kupoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.