Pata taarifa kuu
MAREKANI-RWANDA-BIASHARA

Marekani yaiondolea Rwanda msamaha wa kodi wa nguo

Marekani imeondoa msamaha wa kodi kwa mavazi zote yanayoingizwa nchini humo kutoka Rwanda.

Rais wa Rwanda Paul Kagame na rais wa Marekani  Donald Trump katika mkutano uliopita
Rais wa Rwanda Paul Kagame na rais wa Marekani Donald Trump katika mkutano uliopita REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya Rwanda kupiga marufuku kuingizwa kwa nguo zilizotumiwa nchini nchini mwake maarufu kama mitumba kwa kile inachosema kuwa inaharibu kiwanda chake cha nyumbani.

Hatua hii imetangazwa na mwakilishi wa rais Donald Trump kuhusu masuala ya biashara nchini Rwanda C.J. Mahoney.

Rwanda imekuwa ikisafirisha nguo zenye thamani ya Dola Milioni 1.5 kila mwaka, na hatua hii ya kuanza kutozwa kodi inaelezwa kuwa itaathiri biashara hii.

Serikali ya rais Paul Kagame imekuwa ikisema, mkataba wa AGOA kuhusu kuja kwa nguo zilizotumika kuuziwa kwa raia wake unaharibu uzalishaji katika nchi yake.

Awali, mataifa yote ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kenya, Tanzania na Uganda yalikuwa yameamua kutoruhusu mitumba katika nchi zao lakini, viongozi wa nchi hizo walibadilisha msimamo wao kwa hofu ya kupoteza soko lake nchini Marekani kwa mujibu wa soko la AGOA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.