Pata taarifa kuu
ZIMBABWSIASA-USALAMA

Zimbabwe: Uchaguzi utafanyika, licha ya shambulizi lililomlenga rais

Serikali ya Zimbabwe imesema kwamba shambulio la bomu lililolenga mkutano wa kampeni wa Rais Emmerson Mnangagwa mwishoni mwa juma lililopita halitozuia uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwezi mmoja kabla.

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Bulawayo, 23.06.2018
Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Bulawayo, 23.06.2018 Jekesai NJIKIZANA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kifaa kisichojulikana kililipuka siku ya Jumamosi alasiri baada ya hotuba ya rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa na mgombea wa urais, ambaye alinusurika mbele ya maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika kwenye uwanja wa mji mkubwa wa kusini mwa Bulawayo, ngome ya upinzani.

Watu wasiopungua 49 walijeruhiwa, wengine katika hali mbaya, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na polisi siku ya polisi.

Shambulizi, ambaliohalijadaiwa na kundi lolote, limeitumbukiza Zimbabwe katika hali ya wasiwasi, wakatia mbapo kampeni za uchauzi zilikua zikipamba moto, ikiwa umesalia mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa rais na wa wabunge uliopangwa kufanyika Julai 30.

Mmoja wa makamu wa rais wa nchi hiyo, Constantino Chiwenga, ambaye alijeruhiwa katika shambulizi hilo alisema siku ya Jumapili kuwa kalenda ya uchaguzi haitobadilishwa.

"Hebu tuweke mambo wazi, hakuna kitu kitachozuia kufanyika kwa uchaguzi nchini Zimbabwe, hakuna kabisa," alisema wakati wa hotuba yake mbele ya maelfu ya wa wafuasi wake huko Chitungwiza, katika moja ya vitongoji vya mji mkuu wa nchi hiyo, Harare.

"Kitendo hiki cha ugaidi (...) si chochote, hakitauzuia mtu yeyote," alisema mkuu wa zamani wa majeshi ya Zimbabwe, akiahidi kuwa wahalifu "watakamatwa" na polisi na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Saa chache baada ya shambulizi hilo, Rais Mnangagwa alishutumu, bila kutaja majina , "maadui wake" waliotaka kummalizia maisha. "Kuna majaribio mengi," alisema kwenye televisheni. "Nikawaida yangu(...) lakini ninaendelea."

'Mgogoro wa ndani'

Emmerson Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75 alichukua madaraka baada ya kujiuzulu kwa Robert Mugabe mwezi Novemba mwaka jana.

Siku moja baada ya shambulizi la Bulawayo, wataalamu wanabaini kwamba shambulizi hilo linahusiana na malumbano ya ndani katika chama tawala nchini Zimbabwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.