Pata taarifa kuu
DRC-AMANI-GOMA

Muziki watumiwa kuhimiza amani Mashariki mwa DRC

Tamasha la Amani ambalo limekuwa likifanyika kwa mwaka wa tano sasa Mashariki mwa DRC, kwa lengo la kutumia muziki, kuhimiza amani Mashariki mwa nchi hiyo, limemalizika siku ya Jumapili jioni mjini Goma.

Tamasha la Amani mjini Goma Mashariki mwa DRC
Tamasha la Amani mjini Goma Mashariki mwa DRC amanifestival.com
Matangazo ya kibiashara

Wasanii mbalimbali kutoka DRC na nje ya nchi hiyo, wanatumia nyimbo zao kuhimiza amani katika eneo hilo ambalo miaka ya hivi karibuni, limesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha.

Waasi wamekuwa wakiwavamia raia wasiokuwa na hatia pamoja na maafisa wa usalama wa serikali katika miaka ya hivi karibuni, na kusababisha eneo hilo kuwa hatari.

Juhudi za Umoja wa Mataifa kupitia jeshi la MONUSCO, halijafanikiwa kuleta amani nchini humo tangu mwaka 1999.

Maelfu ya watu waliohudhuria tamasha la amani, mjini Goma
Maelfu ya watu waliohudhuria tamasha la amani, mjini Goma amanifestival.com

Tamasha la mwaka huu, limeshuhudia wanamuziki wenye majina makubwa kama Jose Chameleone kutoka Uganda na Ferré Gola kutoka DRC ni miongoni mwa wanasanii wanaowaburudisha raia wa Mashariki mwa nchi hiyo.

Wakati uo huo, mwanamuziki wa nchi hiyo Black Man Bausi alitoweka siku ya Alhamisi wiki hii katika mazingira ya kutatanisha.

Familia yake inasema haijawasiliana na mwanamuziki huyo lakini wana imani kuwa atarejea salama.

Waandaji wa tamasha hilo wanasema, mwanamuziki huyo alikuwa miongoni mwa wasanii walioburudisha mwaka uliopita.

Tamasha hili la tano linafadhili na Idhaa ya RFI na France 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.