Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Wapiganaji 35 wauawa katika mapigano na jeshi DRC

Jeshi la Serikali ya DRC limesema kuwa jumla ya wapiganaji wa waasi 35 kutoka kundi la Mai Mai linaloongozwa na William Yakutumba wameuawa katika operesheni Sokola ya pili mjini Fizi, huku jeshi hilo likipoteza askari wake 15 na wengine 19 kujeruhiwa.

Jeshi la DRC (FARDC) mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi la DRC (FARDC) mashariki mwa nchi hiyo. Reuters/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Congo linasema limefanikiwa kuwakamata wapiganaji kadhaa pamoja na silaha za kijeshi zilizokuwa zinatumiwa na wapiganaji hao.

Jenerali anayeongoza operesheni hiyo, Jenerali Yav Philemon amesema jumla ya wapiganaji 70 wamekamatwa na wengi walijisalimisha wenyewe na kuthibitisha kujeruhiwa kwa kamanda wa waasi hao Yakutumba na kumkamata naibu wake Ekanda Byamungu.

Jenerali Philemon akayaonya makundi mengi ya waasi ambayo yameendelea kutatiza usalama kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Operesheni ya jeshi la Congo tayari imesababisha maelfu ya raia kukimbia maeneo yao.

Wengi walikimbilia nchi jirani za Burundi na Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.