Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ANC-SIASA

ANC kujadili utaratibu wa kumuondoa madarakani Zuma

Siku moja baada ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kukataa wito wa chama chake wa kujiuzulu kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, chama cha ANC kimeitisha mkutano wa viongozi wake wa juu siku ya Jumatano, Februari 7.

Jacob Zuma, rais wa Afrika Kusini.
Jacob Zuma, rais wa Afrika Kusini. PHILL MAGAKOE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa chanzo kutoka chama cha ANC mkutano huo ni kwa ajili ya kujadili shinikizo la kumtaka rais Jacob Zuma kuachia ngazi.

Lakini katika taarifa iliyotolewa na chama cha ANC kuhusiana na mkutano huo imesema kuwa,wanakutana kujadili kuhusu kukabidhiana uongozi wa chama kutoka kwa Rais Zuma, mwenyekiti wa zamani chama cha ANC na Cyril Ramaphosa ambaye ni kiongozi mpya wa chama hicho.

Rais huyo amekuwa anakabiliwa na shinikizo zaidi kujiuzulu kufuatia mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu katika chama chake cha ANC siku ya Jumapili.

Hata hivyo rais Zuma ameshikilia msimamo wake kutokubaliana na shinikizo la kumtaka aachie madaraka.

Zuma aimekuwa akiandamwa na kashfa za rushwa, ambapo katika miaka ya hivi karibuni alihusishwa na familia yenye asili ya India ijulikanayo kama Gupta ambapo inadaiwa alitumia madaraka yake vibaya ili kujinufaisha yeye na washirika wake hao.

Bw Zuma aliyefungwa gerezani baada ya kuhsiriki katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi anaonekana kuwa katika hatua za mwisho za awamu yake ya pili na ya mwisho kama Rais.

Habari ambazo hazijathibitiwa zinasema kuwa katika mkutano wa Jumapili Zuma aliomba kupata kinga dhidi ya kushtakiwa kwa yeye na familia yake.

Cyril Ramaphosa aliichukuwa nafasi ya kiongozi wa chama cha ANC kutoka kwa Zuma, anayekabiliwa na tuhuma za rushwa.

Wachambuzi wanasema wakuu wa chama hicho wanajaribu kuondoa mvutano wa kung'ang'ania madaraka ambao unaweza kukigawanya chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.

Wanatarajiwa kuanza mchakato wa kumuondoa rais Zuma kupitia mfumo rasmi wa kumuondoa au kwa kuidhinisha hoja bungeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.