Pata taarifa kuu
GUINEA-UCHAGUZI-SIASA

Upinzani kupinga matokeo ya uchaguzi Guinea

Viongozi wa upinzani nchini Guinea mwishoni wametupilia mbali uchaguzi wa serikali za mitaa na kusema kuwa ni ulaghai ulio wazi uliofanyika kwenye nchi hiyo ya Afrika magharibi, na kwamba uchaguzi huo ulicheleweshwa katika sehemu mbali mbali serikali ikilenga kufanya udangayifu.

Maafisa wa Tume ya Uchaguzi (Ceni) wakihesabu kadi za uchaguzi katika kituo cha kupigia kura cha Conakry mnamo Februari 4, 2018.
Maafisa wa Tume ya Uchaguzi (Ceni) wakihesabu kadi za uchaguzi katika kituo cha kupigia kura cha Conakry mnamo Februari 4, 2018. CELLOU BINANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu milioni sita walitakiwa kupiga katika uchaguzi huo wa kwanza, tangu mwaka 2005.

Upinzani unadai kuwa uchaguzi wa Jumapili uligubikwa na udanganyifu mkubwa, utumiaji vibaya wa kura, na kuna watu walipiga kura zaidi ya mara moja.

Lakini Jacques Gbonimy, mmoja kati ya maafisa wa Tume ya Uchaguzi (Ceni), amejaribu kujitetea akisema: "Katika baadhi ya majimbo, baadhi walisema kuwa muda wa kupiga kura uliongezwa hadi 20h. Ceni haikutoa uamuzi huo. Uchaguzi ulikwenda vizuri.

 

 

 

 

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Sidya Toure amewaambia wanahabari kuwa wapinzani wana uthibitisho kuwa Kuna udanganyifu mkuwa ambao ulifanyika katika ngazi ya kitaifa, ambao ulianzia katika vituo vya kupigia kura, hivo hawatakubali matokeo yoyote ya uchaguzi huo.

"Tuna wakuu wa wilaya na wasaidizi wao, walianaweza kuchukua vifaa vyote vya uchaguzi na kuomba kwamba zoezi hilo likafanyikie nyumbani kwao au ofisini kwao. Na waliweza kuzuia kuingia kwa wawakilishi wa vyama vingine, hasa wale wa upinzani. "

Waziri mkuu wa zamani na kiongozi wa chama cha UFR, Sidya Toure.
Waziri mkuu wa zamani na kiongozi wa chama cha UFR, Sidya Toure. AFP PHOTO / CELLOU BINANI

Waziri mkuu wa zamani na mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha UFDG, Cellou Dalein Diallo, amesisitiza akisema: "Nimetoa wito kwa wananchi wanaotaka demokrasia kusonga mbele kupinga mchakato hu wa uchaguzi ambayo Bw Alpha Condé na familia yake wanajiandaa kwa uchaguzi huu wa mitaa.

Makabiliano yalizuka kati ya wapiga kura wa vyama hasimu au wafuasi wa upinzani na polisi nchini kote ikiwa ni pamoja na mji mkuu wakati wa kuhesabu kura au wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.