Dalein Diallo: Rais Conde atakiwa kuheshimu makubaliano na sio kupoteza muda
Upinzani nchini Guinea Conakry unaelekea kufaanikisha harakati za mageuzi nchini humo baada ya kufaulu kuandaa mihadhara ya wazi wakiitaka serikali ya nchi hiyo kutekeleza makubaliano yaliofikiwa kati ya vyama vinavyounga mkono utawala na upinzani mwaka 2016.
Imechapishwa:
Makubaliano hayo yanaagiza kupitia upya sheria ya uchaguzi, ukaguzi wa dafatari la wapiga kura, kuandaa uchaguzi wa serikali za mitaa na kufidia familia za wahanga wa vurugu za kisiasa zilizotokea nchini humo katika miaka yta hivi karibuni.
Katika taarifa iliosainiwa na rais wa Guinea Alpha Conde amewataka washirika wake kutekeleza makubaliano hayo. Tibou Kamara ni waziri katika ikulu ya rais na mshahuri binafasi wa rais Alpha Conde.
Upande wake kiongozi mkuu wa upinzani Cellou Dalein Diallo ambae ametowa wito wa kuandamana Jumatano hii akidai kwamba rais Conde alitakiwa kuheshimu makubaliano na sio kupoteza muda.